12 mbarori kufuatia tukio la kutekwa kwa Mo Dewji

Watu 12 washikiliwa kwaajili ya mahojiano kutokana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘MO Dewji’ hadi sasa idadi inaendelea kuzidi hadi kufikia 12.

Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hadi sasa watu 12 wameshikiliwa ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo lililotokea kwani waliokamatwa ni pamoja na walinzi wa hoteli ya Collesium, mahali ambapo tukio hilo limetokea.

“Kwa sasa wako 12 wakiwamo walinzi wote watano wa Kampuni ya G1 inayosimamia ulinzi wa hoteli hiyo, pia kuna security Manager (afisa usalama) wa hoteli,” amesema Mambosasa