Rais Mugabe aenda nchini Singapore kwa matibabu

Rais wa Zimbambwe Robert Mugabe ameenda nchini Singapore kufanya vipimo vya Afya yake, siku chache baada ya sherehe ya kufikisha miaka 93.

Afya ya kiongozi huyo imekua dhaifu zaidi, na sasa anapata shida hata kutembea wakati wa matukio mbalimbali ya kitaifa.

Msemaji wa rais huyo alisema kuwa vipimo hivyo ni vya mara kwa mara na Rais anatarajiwa kurejea nchini Zimbabwe wiki ijayo.