Rais Barrow awarejesha kazini wanajeshi 18

Rais wa Gambia, Adama Barrow amewarudisha kazini wanajeshi 18 wakiwemo 6 walioshitakiwa kwa kutaka kumpindua Yahya Jammeh mwaka 2014.

Wanajeshi hao 6, walihukumiwa kifo mwaka 2015 na rufaa waliyokata ilikuwa ikiendelea hadi hivi karibuni walipopata msamaha kutoka kwa Rais Barrow.

Uamuzi huu umekuja siku chache baada ya Rais huyo kumbadilisha Mkuu wa Majeshi, Ousmane Bargie aliyekuwa akimsapoti Rais aliyepita na kumuweka Luteni Jenerali Masanneh Kinteh.