ANC kutangaza mjadala mpya wenye lengo kubadilisha sera

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimetangaza mjadala mpya wenye lengo la kufanya mabadiliko ya baadhi ya sera ili kuboresha utendaji wa chama hicho katika jamii, uchumi, na siasa.

Mkuu wa sera wa ANC Jeff Radebe amesema, Muswada wa Majadiliano ya Mageuzi ya Kiuchumi, ambao kwa sasa unapokea maoni kutoka kwa jamii, unatarajiwa kuwa kwenye ajenda za Mkutano wa Kitaifa wa Kisera wa ANC uliopangwa kufanyika Juni 30 hadi Julai 5. Amesema kuwa chama hicho kitashuhudia mabadiliko kutoka uwezeshaji wa kisiasa hadi uhuru wa kiuchumi na kijamii, ambao unaweza kutimizwa kupitia mageuzi makubwa ya kiuchumi.

Chama hicho pia kinadhamiria kuwawezesha wajasiriamali weusi kuanzisha biashara na mashirika madogo, na kusimamia vyema sekta binafsi ili kuepuka ukiritimba wa bei, ushindani usio wa usawa, na vitendo visivyo vya usawa katika sehemu za kazi.