Jonas Mkude wa Simba apata ajali

Kiungo Jonas Mkude ambaye hapo jana aliisaidia timu yake kutwaa taji la Azam Sports Federation Cup amepata ajali ya gari wakati akiwa safarini kurejea jijini Dar es Salaam.

Pichani ni Jonas Mkude

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mtibora, Dumila Mkoani Morogoro baada ya tairi la nyuma kupasuka. Taarifa za awali zinasema yeye pamoja na majeruhi wengine wamepelekwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.