Paul Pogba aanza Ramadhan kwa kufanya Umrah Makkah

Kiungo ghali Duniani na Supastaa wa Klabu ya Manchester United ambaye ni takriban siku nne zilizopita aliiwezesha timu yake kutwaa taji la Europa League, Paul Pogba amewasili Makkah Saudia Arabia kufanya ibada ya umrah.

Pogba ameonekana katika picha zilizoekwa katika tandao wa Twitter akiwa amevaa mavazi yanayovaliwa katika ibada za Hijja na Umrah huku akiwa tayari kuanza kwa ibada hiyo.

Paul Pogba akiwa tayari kuanza ibada ya Umrah huko Makkah ndani ya siku ya mwanzo ya mwezi Mtukufu wa Ramdhan
Mchezaji wa Manchester United akiwa ndani ya Makkah kuhudhuria ibada ya Umrah ndani ya weiz huu mtukufu wa Ramadhan

Mapema, Pogba alitumia ukurasa wake wa Instagram kuweka video vifupi kimuonesha akiwa na begi na pia aliandika “Njiani kwenda kutoa shukrani kwa msimu huu, Tutaonana baadae Manchester”

Umrah ni moja ya ibada katika Dini ya uislam ambayo inafanana na ibada ya Hijja ila tofauti na Hijja hii si ya lazima kuifanya na hufanywa wakati wowote mtu anapojisikia.