Tanzia: Shabiki wa Simba afariki Dunia kwa Ajali

Shabiki mkubwa wa klabu ya Simba amefariki kwenye ajali ya gari ambamo kiungo Jonas Mkude alikuwemo wakati wakitokea Dodoma kurejea Dar es Salaam.

Shabiki huyo ambaye pia ni mwanachama wa klabu ya Simba Shose amefariki dunia baada ya kupata majeraha makubwa kutokana na ajali hiyo.

Gari iliyopata ajali ambamo alikuwemo Marehemu Shose pamoja na Jonas Mkude
Shose enzi za Uhai wake