Je kuna ugumu kuwa mwanasoka muislam katika mwezi wa Ramadhan?

Dunia imeshuhudia mara kadhaa uwepo wa Wachezaji nyota wa kiislam wakiwa katika mashindano makubwa huku wakiwa wapo katika mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Mfano ni hapo juzi tu Simba SC ilipokuwa ikicheza fainal na Mbao FC  katika kombe la shirikisho la Azam huku ikiwa ni Ramadhan na ndani ya vikosi hivyo kukiwemo nyota mbalimbali tegemeo ambao ni waislam akiwemo mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania bara Mohammed Hussein TShabalala.

Hayo pia yalijitokeza mwaka jana (2016) katika michuano ya kombe la Ulaya (EURO) ambapo michuano hiyo iliangukia katika mwezi wa Ramadhan huku kukiwepo wachezaji wakubwa mbalimbali waislam kama Paul Pogba, Emre Can, Sami Khedira na Mesut Özil, bila kusahau timu nzima yaUturuki.

Wengi tumekuwa tukijiuliza, Je wachezaji hawa huwa wanafunga?, wanawezaje kucheza soka bila kuathiri imani ya dini yao ya kiislam?, Je wanakutana na vikwazo gani toka waajiri wao ambao wanataka wacheze mpira wakiwa katika hali nzuri bila kuchukulia kama wamefunga au la?

BBC ilifanya mazungumzo na Nathan Ellington, Mchezaji wa Zamani katika ligi kuu ya Uingereza akikipiga na timu za Wigan Athletic, West Bromwich Albion, Derby County na Watford. Aliingia katika Uislam akiwa na umri wa miaka 23. Mazungumzo yake na BBC yalihusu changamoto wanazokumbana nazo wachezaji waislam hasa katika kipindi cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Baadhi ya wachezaji huwa hawafungi wanapokuwa katika mashindano. Nini muongozo juu ya hili?

Kila Muislam, mtu mzima anatakiwa na ni lazima afunge, lakini kama una safiri au unaumwa, hapo unaweza kuamua kuja kufunga siku nyingine

Linapokuja suala la michuano ya Ulaya (EURO), inakua sio tatizo sana kwasababu kila mtu anasafiri. kwahiyo kama mchezaji anaamua kutofunga basi ana muda wa mwaka mzima kuja kuifunga iyo siku.

Je kuna kuwa na kubezwa kwa mchezaji yeyote anae amua kuja kufunga baadae kutoka kwa waislam?

Hilo linaweza kutokea tu endapo mchezaji ataacha kufunga huku akiwa anacheza akiwa katika mji wake. Kwa maana kwamba atakua hajasafiri, hivyo hata sheria ya kutokufunga hapo haitumiki.

 

Je uliwahi kukutana na changamoto kutoka kwa Kocha au uongozi wa Timu wa kukutaka kutofunga kipindi cha ratiba ngumu ya mashindano?

Ndio. Nilikua na kocha ambaye alinambia kuwa hanipangi katika timu kwasababu nimefunga. Aliniambia kufunga kunaathiri stamina yangu, uwezo na kiwango changu cha nguvu.

Kuna wakati nilikua nafunga bila ya timu yangu kujua – sikuwaambia. Na uzuri ni kwamba ilikua huwezi kuona tofauti yoyote. Nilipocheza Ugiriki, mchezaji mmoja alinitania kuwa nifunge siku zote kwasababu nilikua nacheza vizuri.

Hii inategemea tu na wewe mwenyewe unavochukulia. Uwezo wako wa kucheza mpira ukiwa umefunga unatokana na wewe mwenyewe unavoichukulia iyo hali. Ndio kuna watu wanaathirika katika uwezo wao. Na ikitokea ukaanza kusikia kizunguzungu or ukijisikia vibaya basi ni lazima ule.

 

Je ilikua sawa kwa kocha kutokupanga ucheze ukiwa umefunga? 

Sidhani kama ilikua sawa kwa suala langu mimi. Kama nilivosema kuna wakati nilikua nafunga bila timu kujua na hakuna aliehisi chochote. Na nilikuja kuiambia timu hilo.

Naelewa kuwa mtizamo wa kocha anapojua kuwa mchezaji wake amefunga. Simlaumu kabisa kwa hilo lakini nadhan makocha wanapaswa kutambua kila mtu yupo tofauti. Inatakiwa watizame kila mtu na mtu. Wachezaji tofauti wanakuwa tofauti.

Ni vipi ulikuwa unajipanga katika mfungo?

Nilikuwa nahakikisha kuwa napata vyepesi vyenye kutia nguvu wakati wa Kuftari kama uji, ndizi na pia vinywaji kwa wingi.