Mradi wa ‘Fursa Kijani’ Mkombozi wa Vijana Zanzibar

Tukiwezeshwa tunaweza ni msemo maarufu hasa kwa wanawake ambao wanajishughulisha na ujasiriamali kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Lakini msemo huu unatafsiriwa vizuri hapa Zanzibar ambapo vijana zaidi 70 wamewezeshwa ili kupata muelekeo kuwa wazalishaji wazuri kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na familia zao.

Vijana hao ambao awali walikuwa wamekata tamaa kwa kukosa jambo la kufanya ili kujikwamua kimaisha walitafutwa kwa njia mbali mbali ili kupewa elimu ya uzalishaji wa aina mbali mbalin ikiwemo Kilimo hai (kilimo asili) ambacho hakitumii kemikali, ufugaji wa Nyuki pamoja mbolea ya kiasili mradi ambao unajuilikana kwa jina la Fursa kijani.

Mafunzo hayo ambayo yanatolewa yanakuwa na lengo la kuwashajihisha vijana kujishughulisha na kilimo hai (Kilimo asili) na kuacha kujishughulisha na kilimo cha kisasa ambacho kinatumia mbolea za kemikali kwa madai ya kuwa  kinaharibu Mazingira na Afya za Binaadamu.

 Bernadette Kirsch ambaye ni Muanzilishi wa Practical Permaculture Institute ya Zanzibar ambayo inawasomesha vijana hao kwa udhamini wa taasisi ya milele Foundation Zanzibar alieleza kuwa wanataka kujikita katika kuleta matokeo mazuri yenye faida kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Mkurugenzi Mtendaji Fumba Town Service Center Sebastian Dietzold akitoa maelezo ya nafasi ambazo huwapatia vijana mara ya kuhitimu masomo yao katika Chuo cha Practical Permacuture Institute of Zanzibar ambapo wanafunzi wake hupata Udhamini wa Milele Foundation

Alieleza kuwa vijana wakishapata elimu hiyo wanaombwa kuwasaidia wengine ili waweze kujikwamua kimaisha kupitia mradi huo Fursa Kijani.

Milele Foundation Zanzibar kwa sasa ndio inayofadhili mradi wa “Fursa Kijani”  ambao ulizinduliwa mwaka 2016 kutengeneza fursa kwa  vijana wavulana na wasichana ”ambao hawapo mashuleni” Kupitia kazi za kijani wanapata uwezo na ujuzi wa vitendo na pia kuunganishwa na wanufaikaji wa mradi na ujuzi halisi wa kazi.

Akizungumza na Tanzania daima Mratibu wa Mradi kupitia taaisisi ya Milele Foundation Zanzibar Bi Khadija Shariff alisema kuwa Vijana hao hupata ufadhili wa kila kitu kwa wiki mbili ambao unawasiadia kulala hapo hapo kwenye eneo la mafunzo.

“Lengo kutoa Full scholarship ni kutaka tuwawezesha vijana kikamilifu ili waweze kutoka na kitu ambacho tumekikusudia kwa ajili yao na nchi yao” alieelza Bi Hadija.

Alieleza kuwa mradi huo ni wamajaribio ambao ukifanikiwa unalengo la kuwachukua vijana wengi wazanzibar ili kujenga taifa lenye vijana imara na maisha bora.

“Tunataka tutoe timu bora ambayo itapelekea kupata na jimii iliyo imara” alieleza Khadija Shariff.

Alifahamisha kwamba  Mafunzo yanajumlisha wiki mbili za kujifunza mambo mbali mbali ikiwemo kilimo endelevu, miezi mitatu ya kujifunza kazini katika kituo cha Fumba Town Service Center (FTSC).

Licha ya kazi hiyo Milele inaeleza jinsi ilivyopata changamoto kwa mwaka wa mwanzo ambapo baadhi ya vijana walikimbia kabla ya masomo kwisha.

“Lakini tuligundua wale vijana walikuwa na shghuli nyengine ndio ikawa hawakuwa na kitulizano pale chuoni lakini kwa sasa tumejipanga vizuri” alieleza Khadija.

Alieleza changamoto nyengine ambayo wanakabiliana nayo ni kutokana kuwa vijana wanawachukua ni kutoka katika familia masikini sana na  sasa wanategemea kila kitu kwao wao na kudai lakini na wao wamejitahidi kuzitatua na sasa halin inakwenda vyema.

Kituo hicho FTSC kimeonekana kutoa mchango mkubwa kwa vijana hao kwani mara wanapoamaliza mafunzo kutoka katika chuo cha Practical Permaculture Institute of Zanzibar huwachukua wahitimu hao na kuwapati mafunzo kwa vitendo kwa muda wa miezi mitatu.

Mara baada ya kumaliza mafunzo hayo ya vitendo huwafanyia usaili wahitimu hao na baadae huto ajira kwa wale ambao watafaulu usaili huo ambapo kwa sasa tayari imeshaajiri vijana 30 kutoka kwenye mradi wa Fursa kijani kati ya wale zaidi 70 na wengine wamepata ajira kutoka sehemu nyingine kama vile  mahoteli.

Akizungumza na muandishi wa habari hizi huko afisini kwake Fumba nje ya mji wa Zanzibar ambao una umbali wa karibuni kilo mita 25 kutoka mjiku wa Zanzibar Mkuruegenzi Mtendaji Sebastian Dietzold  alieleza kuwa lengo lao kuwachukua vijana hao ni kutaka kufikia malengo ya taasisi yake ya kujenga Nyumba bora.

“Sisi tunajenga nyumba ambayo yatakuwa ni makazi bora , lakini kama hakuna maisha mazuri, lile lengo tumefikia hamna” alieleza Dietzold.

Mwaandishi wa Habari hizi akifanya mahojhiano na wahitimu wa Mafunzo mbali mbali katika mradi wa Fursa Kijani ambao hufadhiliwa na Milele Foundation.

Alieleza kuwa wanawawezesha vijana hao ili maisha yao yawe ya kisasa ambayo yatategemea zaidi kilimo hai (Kilimo Asili) ambacho hakina athari kwa binaadamu.

Alieleza kuwa licha ya vijana wengi awali walikuwa hawana uwezo wala fikra zozote zile, na kueleza kuwa katika taasisi yake anajivunia vijana wengi ambao wamepata masomo hayo na kuzalisha vitu vya aina tofauti.

“Nawaomba vijana wote ambao hawana uwezo wajitokeze na watawezeshwa ili na wao waweze kujikwamua kwani fursa zipo nyingi hasa wakishapata ujuzi” alieleza Dietzold.

Muharami Ali Hamad ni miongoni mwa vijana ambao walipata mafunzo hayo kupitia mradi huo wa Fursa kijani ambapo leyo anazishukuru taasisi hizo hasa akieleza thamani yake kubwa kwa Milele Foundation Zanzibar ambayo ndiyo iliyomdhamini kupata ujunzi ambao anao.

“Leo unapo niona hapa kakaangu nafanya kitu ambacho katika akili yangu kawaida hakikuwemo namshukuru mola wangu halafu  sasa nisipoishukuru taasisi hii nitakosa radhi zake” alieleza Hamad.

Hamadi ambaye anafanyakazi katika kituo cha Fumba Town Service Center kitengo chake ni kufuga Asali ya kisasa ambayo inatumia utaalamu wa hali ya juu tofauti na ile iliozoeleka.

Kwa upande wake Bi Ujudi Ali Khamis ambaye yeye anafanyakazi katika kituo cha kutengeza mbolea hai ( mbolea Asili) alieleza kuwa ni wakati wake sasa kuwapitia wanawake wenzake na kuwashawishi waweze kujiunga na chuo ili baadae waweze kuwa na taifa ambalo vijana waliowengi wanaweze kujitegemea.

Alieleza kwa sasa kazi yake katika taasisi hiyo ni kutengeza mbolea na kueleza anapotoka kazini hua anatoa elimu kwa wenzake mitaani .

Akieleza Mkurugenzi wa maendeleo ya Vijana kupitia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) Mwanaidi Muhamed Khamis aliwashauri vijana hao kuyatumia vyema mafunzo hayo kwa kile alichodai kuwa furaha ya SMZ ni kuonan vujana wanapata maisha yaliobora kwa ajili ya maendeleo ya taifa.

Haya ni maendeleo makubwa katika taifa kupitia fikra hii ambayo ilibuniwa na taasisi hizo tatu ambapo kama jamii itaitumia vile ilivyo ndivyo basi vijana wengin watakuwa watalamu wa uzalishaji wa vitu mbali mbali.

Jamii inatakiwa kuchua hii ni fursa adimu ambayo ni ngumu kupatikana na hivyo kuacha kuingiza siasa na kuchukua wale walengwa waliokusudiwa.