Zanzibar ipo hatarini kukosa asali kutokana na nyuki kukimbia kwa kukosa makazi
Wakulima na Wafugaji wa nyuki katika mkoa wa kusini unguja wamesema Zanzibar ipo hatarini kupoteza rasilimali nyuki kutokana na uharibifu mkubwa wa ukataji misitu unaofanywa na baadhi ya wananchi.
Akizungumza mara baada ya zacca kufanya ziara katika kuwakagua wafugaji wa nyuki huko Kitogani Mwenyekiti wa Jumuiya ya ufugaji wa nyuki Zaba Salum Rashid Juma amesema nyuki wamekuwa na faida kubwa katika uzalishaji wa asali lakini uwepo wa athari za mabadiliko ya tabianchi kumesababisha nyuki kutoweka na kupunguza uzalishaji wake jambo linalowapa wakati mgumu wafugaji mbalimbali katika kukabiliana na matatizo hayo kwani hupoteza kipato chao.
Hata hivyo ametoa wito kwa serikali kuona umuhimu wa kuelimisha jamii hasa wa vijijini wanaotegemea rasilimali msitu msitu kwa shughuli zao za kujikimu kimaisha,kupanda miti na kutafuta njia mbadala ya kujiendeleza kiuchumi ili msitu kubaki kuwa hadhina na kuwa makaazi ya wadudu wakiwemo nyuki na vipepeo kwa maendeleo ya Zanzibar.
Bei ya asali imekuwa ikiuzwa lita Elfu 30 hadi 40 ambayo hutumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo chakula,dawa na mambo mengine.
Na: Amina Omar Zanziabr24.