Mfanyabiashara wa silaha maarufu afariki dunia

Mfanyabiashara wa silaha maarufu duniani Adnan Khashoghi mwenye umri wa miaka 82 ambaye ni tajiri anayefahamika kwa maisha yake ya kifahari amefariki kwa maradhi ya kutetemeka.

Familia yake imeeleza kuwa Khashoghi amefariki jumanne june 06, 2017  wakati akipatiwa matibabu ya maradhi ya kutetemeka huko mjini London.

Mfanyabiashara huyo alikuwa mmoja kati ya watu matajiri zaidi duniani miaka ya 1970 na 80 kwa kupata kandarasi za kimataifa za kuuza silaha, hadi kuthubutu kuwakilisha ufaransa katika mbioa dhidi ya Uingereza ya kushinda kandarasi ya dola bilioni 20 kuiuzia Saudi ASrabia silaha, kandarasi iliyopo hadi sasa.

Mnamo mwaka wa 1980 Khashoghi alitumikia kifungo cha gerezani inchini Uswisi kwa tuhuma zakumsaidia aliyekuwa rais wa Ufilipino Ferdinand Marcos kuficha pesa.

Miongoni mwa vitu vya thamani alivyo wahi kumiliki bwana Khashoggi ni pamoja na mashua kubwa zaidi duniani iliyokua ikiitwa NABILA ambayo ilitumiwa katika filamu ya James Bond ya Never Say Never Again, na baadae kuiuza kwa thamani ya dola milioni 29,000 kwa Donald Trump ambaye ni rais wa Marekani kwa sasa miaka ya 1980.

Matatizo ya kifedha katika biashara yake ndio Sababu iliyo pelekea kuiuza mashua hiyo.