Miili na Mabaki ya ndege iliyopotea jana yakutwa Baharini

Miili na mabaki ya iliyokuwa ndege ya kijeshi ya Myanmar iliyoripotiwa kupotea jana jioni yamekutwa mapema leo. Ndege hiyo iliyokuwa imebeba watu 122 wakiwemo wanajeshi, wanafamilia na wahudumu wa ndege ilipotea jaan jioni katika ukanda wa bahari ya Andaman.

Miili mitatu ikiwemo ya watu wazima wawili na mtoto mmoja, imekutwa na jeshi la wanamaji kilomita 35 kutoka pwani ya kusini ya mji wa Launglon, imesema taarifa iliyotolea kupitia ukurasa rasmi wa facebook wa jeshi la Myanmar.

Gurudumu la ndege ambalo linaaminika limetoka katika ndege ya kichina ya Y-8-200F pia lilikutwa katika mabaki hayo.