QS yataja vyuo vikuu bora zaidi duniani mwaka 2017

Shirika la QS Word University Rankings ambalo hutoa orodha ya vyuo vikuu bora Duniani kwa mwaka 2017 chuo kikuu cha Massachusetts Institute of Technology (MIT) cha Marekani bad0 kinachukua nafasi ya ushindi.

Vyuo vikuu vya Stanford na Harvard – pia kutoka Marekani – kadhalika vimeendelea kushikilia nafasi ya pili na ya tatu mtawalia. Na kwaupande wa East Afrika University of Nairobi na Makere University vimechukua nafasi ya 701, Orodha hiyo ilishirikisha vyuo vikuu karibu 1000 duniani kote.

Vyuo vikuu hupimwa kwa mambo kama vile majarida na vitabu vya kisomi vilivyochapishwa, makala zilizonukuliwa, maoni ya wasomi pamoja na waajiri na pia ushiriki wa vyuo vikuu hivyo katika ngazi ya kimataifa.

Vyuo vikuu 10 bora zaidi duniani kwa mujibu wa QS World University Rankings

  1. Massachusetts Institute of Technology (MIT)
  2. Stanford
  3. Harvard
  4. California Institute of Technology (Caltech)
  5. Cambridge
  6. Oxford
  7. University College London
  8. Imperial College London
  9. Chicago
  10. ETH Zurich