Watuhumiwa wa kesi za udhalilishaji sasa kunyimwa dhamana

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe. Haroun Ali Suleiman amesema   kutokana na kuongezeka vitendo vya udhalilishaji Zanzibar kwa wanawake na watoto, endapo serikali kupitia taasisi zake zinazoshughulikia  kesi za udhalilishaji itamkamata  mtu yoyote   na kesi za udhalilishaji haitampa dhamana  mtuhumiwa wa vitendo vya udhalilishaji.

Akizungumza na Waandishi wa Habari huko ofisini kwake mazizini wakati akitaja vipaumbele vya wizara yake kwa mwaka 2017/2018 amesema jitihada mbalimbali zinachukuliwa kuhakikisha kesi za udhalilishaji zinapungua Zanzibar na moja wapo ni ya kuwanyima dhamana watuhumiwa ili kutoa fundisho kwa wengine na kuimarisha utowaji wa haki.

 

Na: Amina Omar Zanzibar24