Maelfu waandamana kudai haki za wapezi wa jinsia moja Marekani

Maelfu ya watu wameandamana katika kile wanachokiita kudai haki za watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja mjini Washington, nchini Marekani.Yanatajwa kuwa maandamano makubwa kuwahi kushuhudiwa tokea kuingia madarakani kwa Trump.Wengi wao wanadai kwamba wanapata vitisho na hawajui mustakabali juu ya maisha yao.

Hata hivyo nao watetezi wa haki za binaadam wanasema bado wanatengwa katika masuala kama ajira.

Maandamano haya yamekuja karibia mwaka mmoja baada ya watu 49 kuuawa kwa kupigwa risasi kwenye klabu moja ya usiku ya watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.