Zaidi ya magari 100 yakamatwa na bima bandia Zanzibar

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA imesema kumekuwa na udanganyifu  na ongezeko la bima bandia nchini kunakosababisha  kupotea kwa mapato ya serikali hivyo mamlaka imezindua mfumo wa Tehama  utakaoweza kusaidia kugundua na kuondoa bima bandia  zisizo na vigezo ili kuepusha upotevu huo.

Akizungumza katika Mkutano na Askari wa usalama barabarani Mkurugenzi wa Maendeleo  ya Masoko na Utafiti wa mamlaka hiyo Adelaida Muganyizi amesema kuna wimbi kubwa la udanganyifu wa bima kwa madereva wa daladala na gari za binafsi kughushi stika za bima na kusababisha hasara kubwa kwa serikali hivyo  mfumo huo wa Tehama utawasaidia Maaskari wa usalama barabarani katika utekelezaji wa majukumu ya kazi yao kuweza kuwabaini  madereva waliofanya udanganyifu na kuwafikisha katika vyombo vya kisheria.

Kwaupande wake Naibu Kamishina wa Usalama barabarani Mkadam Khamis Mkadam ametoa wito kwa Jeshi la Polisi hasa usalama barabarani  kufanya kazi kwa mujibu wa sheria pindipo watakapo mkamata  dereva na bima bandia au kughushi bima kumfikisha katika vyombo vya kisheria na kuwacha kufanya kazi kwa mazoea.

Nao madereva wa madaladala pamoja na madereva wa gari binafsi Omar Ali Wakizungumza na Zanzibar24 katika ziara ya ukaguzi wa magari  yenye bima bandia  wamesema  wamelipokea zoezi hilo kwa masikitiko makubwa kutokana  bado hawana uwelewa wa bima halali na bandia kwani bima zao wanakata katika shirika la bima zanzibar na kwenye matawi ya bima yaliyo karibu yao.

Zaidi ya Magari 100 yamekamatwa la mamlaka ya bima wakati wa ukaguzi wa bima bandia huko maruhubi.