Waziri wa Mambo ya ndani aanza kuwashughulikia waliotajwa katika ripoti ya mchanga wa madini

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewazuia wote waliotajwa kwenye ripoti ya pili ya mchanga wa madini kutoka nje ya mipaka ya Tanzania hadi vyombo vya dola vitakapofanya kazi yake kwa mujibu wa agizo la Rais John Pombe Magufuli.

Waziri mwigulu ametoa taarifa hiyo hiyo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii kwa kuandika “Hakuna uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao. Hongera sana Mh. Rais kwa uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu. Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu.