Taarifa rasmi ya ajali ya gari iliyotumbukia kwenye daraja

Gari aina ya fuso yenye namba Z 880 EF imepata ajali katika daraja la kitope wilaya ya kaskazini B baada ya kufeli break kulikopelekea kuacha njia na kutumbukia katika daraja la hilo.

Tukio hilo limetokea jana juni 13, 2017 majira ya saa nne na dakika hamsini asubuhi, wakati gari hiyo ilipokua ikitokea kazole na kuelekea mto mchanga.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa kaskazini unguja  Hasina Ramadhan Taufiq amewataja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni Dereva Mbaraka Mohammed Khamis mwenye umri wa miaka 50 mkazi wa mfenesini, mwengine ni Emmanuel Maganga Charles miaka 26 mkazi wa Bububu na Ali Mohammed Juma miaka 29 mkazi wa Donge. Majeruhi wamelazwa katika hospitali ya Mnazi mmoja na hali zao zinaendelea vizuri.