Mamlaka ya usimamizi wa Bima Tanzania yatoa mafunzo ya bima halali kwa jeshi la polisi Pemba

MENEJA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania ‘TIRA’ kanda ya Zanzibar Mohamed Ameir, akizungumza kwenye mafunzo ya siku moja, ya utambuzi wa bima halali na isiohalali, kwa watendaji wa Jeshi la Polisi, yaliofanyika skuli ya sekondari Madungu mjini Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 

MENEJA wa ‘TEHAMA’ kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA, Aron Malaki akiwaeleza watendaji wa Jeshi la Polisi Pemba, jinsi ya kuitambua bima halali, kwenye mafunzo ya siku moja yaliotayarishwa na ‘TIRA’ na kufanyika skuli ya Sekondari mjini Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 

WATENDAJI wa Jeshi la Polisi kutoka Mikoa miwili ya Pemba, wakisikiliza njia sahihi za kuitambua bila halali, kwenye mafunzo ya siku moja yaliotayarishwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania ‘TIRA’ na kufanyika skuli ya sekondari wa Madungu mjini Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 

MWANDISHI wa Shirika la Utangazaji Zanzibar Raya Ahmada Mohamed, akisoma ujumbe kwenye simu yake ya mkononi, mara baada ya kutuma namba ya bima, na kugundua kuwa namba hiyo ya bima ni halali, kwenye mafunzo ya utambuzi wa bila halali, yalioandaliwa na Mamlaka ya Usimami wa Bima Tanzania ‘TIRA’, na kufanyika skuli ya Sekondari Madungu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 

ASKARI wa kikosi cha usalama barabarani ambae hakupatikana jina lake, akisoma ujumbe kwenye simu yake ya mkononi, mara baada ya kutuma namba ya bima, na kugundua kuwa namba hiyo ya sio halali, kwenye mafunzo ya utambuzi wa bila halali, yalioandaliwa na Mamlaka ya Usimami wa Bima Tanzania ‘TIRA’, na kufanyika skuli ya Sekondari Madungu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 

MKUU wa kikosi cha Trafiki mkoa wa kusini Pemba ‘RTO’, Shawali Abdalla Ali, akitoa neno la shukuran, mara baada ya kumalizika kwa mafunzo juu ya utambuzi wa bima halali, yalioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania ‘TIRA’, na kufanyika skuli ya sekondari ya Madungu mjini Chakechake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).

 

MKURUGENZI wa masoko na utafiti kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania ‘TIRA’, Adelaida Muganyizi akifungua mafunzo ya siku moja, kwa watendaji wa jeshi la Polisi, juu ya kuitambua bima halali, mafunzo hayo yaliofanyika skuli ya sekondari Madungu na kuwahusisha watendaji wa jeshi la Polisi, (Picha na Haji Nassor, Pemba).