Kiganja aibukia uchaguzi wa TFF

Baraza la michezo la Taifa limeiandikia barua shirikisho la soka la Tanzania TFF kwa kile ilichodai kutotaarifiwa kuhusiana na uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo.

Kupitia barua hiyo iliyoandikwa na katibu mkuu wa baraza hilo, Bw. Mohammed Kiganja limeitaka kamati ya Utendaji ya TFF kukutana na kamati ya nidhamu, rufaa na usuluhishi ya baraza hilo Julai 1 saa nne asubuhi ili kujadili na kupanga taratibu za kufanikisha jambo hilo bila kuvunja misingi ya sheria, kanuni na taratibu za nchi zilizopo.