Nedy ajitoa lawamani

Msanii wa muziki Nedy amekiri  kwa kudai kuwa sio kweli kwamba alitoa kauli ‘wasanii wa Zanzibar waache kulalamika’ ambayo ilitafsiriwa vibaya na baadhi ya wasanii.

Nedy Music alidai kauli ambayo aliitoa aliwataka wasanii wa Zanzibar kufanyakazi kwa bidii.

Alisema aliwataka wafanyekazi kwa nguvu zao zote kwa sababu mbona kuna wasanii wa kule kipindi cha nyuma walifanya vizuri sana. Kwahiyo naweza kusema mimi sikuwaongelea vibaya nilikuwa nataka kuonyesha kila kitu kinawezekana hata huku bara kuna wasanii wengi wakali lakini hawafanyi vizuri.

Alisema ingawa yupo chini ya label ya PKP ya Ommy Dimpoz lakini yeye binafsi nje ya label hiyo anajaribu kufanyakazi kwa bidii zaidi.

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Dozee’.