Watendaji mabaraza ya vijana watakiwa kuacha kujigawa kimatabaka

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amewataka watendaji  wa baraza la vijana Zanzibar  kuwa na mashirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao  ya kazi katika baraza  na kuwacha tabia ya kujigawa matabaka jambo litalopelekea  kuvuruga umoja wao wa kuliletea taifa maendeleo.

Akizungumza katika mkutano na baraza la vijana wa kupitisha mikakati na kanuni za baraza zitakazosaidia katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku amesema ili baraza liwe imara lazima  watendaji  kupitisha mikakati imara pamoja na kanuni itakayowasaidia   kujenga  na kuimarisha maendeleo ya vijana  na taifa zima.

Hata hivyo amesema  Serikali inalengo la kuwawezesha  vijana kiuchumi ili kuweza kujikwamua na hali ngumu ya maisha kwa kutumia fursa zilizopo ambapo lazima vijana kuwa na moyo wa kizalendo wa kujitolea katika kupeleka mbele maendeleo ya taifa.

Kwaupande wake Katibu Mtendaji wa baraza hilo Khamis Faraji Abdalla Akizungumza na mwandishi wetu  nje ya mkutano huo amesema mpango huo wa kupitia na kupitisha mpango mkakati wa baraza la vijana na kupitisha kanuni za uongozi na utawala utawasaidia viongozi jinsi ya  kuyaongoza mabaraza ya vijana kwa mujibu wa  kisheria na kanuni za kiuwendeshaji wa mabaraza hayo.

Mkutano huo wa baraza la vijana  ni wapili kufanyika zanzibar.