Mtoto wa Afrika

Ikiwa leo ni siku ya maadimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ni wajibu kwa kila mzazi, mlezi, kufahamu vipengele tofauti vinavyomuhusisha mtoto kupata haki zake pamoja na malezi  bora ndani ya mzunguko mzima wa maisha..

Watoto wanayo mahitaji ya msingi ambayo kote Duniani yanatengeneza ‘haki’ haki za mtoto huwa ni wajibu wa mtu mzima kutimiza mahitaji ya mtoto ili awe mwenye afya, apate elimu na ashiriki katika ujenzi wa nchi yake sasa na hasa atakapokuwa mtu mzima.

Ni vyema ikaeleweka kwamba tunapozungumza kuhusu watoto, tunazikusudia jinsia zote mbili. Yaani watoto wa kiume sambamba na wale wa kike.

Katika Uislamu hakuna chembe ya ubaguzi, watoto wote wana haki sawa kwa wazazi wao kwa mujibu wa sheria.

 

Mtoto ni mtu aliye na umri chini ya miaka kumi na nane. Ustawi wa mtoto; yaani, furaha na amani kwa mtoto itapewa kipaumbele katika kutathmini mambo yote yanayomhusu mtoto, yawe yamefanywa na taasisi ya Ustawi wa Jamii,  serikali au binafsi, mahakama au vyombo vya utawala.

Miongoni mwa mambo muhimu ambayo mtoto anastahiki kupatiwa kama ifuatavyo:

Haki ya Kutokutengwa :

Mtoto atakuwa na haki ya kuishi huru bila kuwapo na namna yoyote ya kutengwa; yaani kuonekana kuwa hastahili kujumuika na wenzake katika kundi.

Mtu hatakiwi kumtenga mtoto kwa sababu anaongea lugha tofauti. Mtoto hatakiwi kutengwa kwa sababu ametoa maoni tofauti ya kisiasa  jinsia rangi umri au dini.

Mtoto ana haki ya kuishi na wazazi au walezi wake.

Mtu yoyote haruhusiwi kumnyima mtoto haki ya kuishi na wazazi, walezi au familia yake. Pia ni haki ya mtoto kukua katika malezi na mazingira ya amani kwa kujiskia huru pasi na kutokua na wasiwasi muda wote kwani husababisha madhara makubwa kwa mtoto, hasa pale ambapo mtoto ananyanyaswa.

Kwa kufuatana na sheria na taratibu zinazotumika, Mamlaka yenye uwezo, mfano, Serikali ya Mtaa au mahakama inaweza kuamua kwamba mtoto atenganishwe na wazazi, kwa sababu ya ustawi wake Ikitokea hivyo mtoto lazima apewe malezi mbadala.

Wajibu wa kumtunza mototo.

Ni wajibu wa mzazi, mlezi au mtu yeyote mwenye kumlea mtoto kutoa matunzo kwa mtoto. Wajibu huu hasa unampatia mtoto haki ya: Chakula, Malazi, Mavazi, Dawa pamoja na chanjo, Elimu na maelekezo au mafunzo, Uhuru na  Haki ya kucheza na kupumzika.

Tuwatunze watoto kwa kujenga taifa la badae.