Tahadhari juu ya maradhi ya kipindu pindu

Jamii imetakiwa kuchukua tahadhari  juu ya suala zima la kujikinga na maradhi ya  kipindupindu katika  kuelimisha jamii na taifa zima kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Afisa wa Afya Wizara ya Afya Juma Muhammed Juma wakati akizungumza na waandishi wa habari huko kidongochekundu Wilaya ya Mjini Unguja.

Amesema ni vizuri Waandishi wa vyombo vya habari kuwa na uelewa juu ya maradhi ya kipindupindu kwani inapelekea jamii kujenga uelewa mkubwa juu ya maradhi hayo.

Hata hivyo ameyataja maeneo ambayo yanakusanya idadi kubwa ya wagonjwa wa kipindu pindi ni Mkoa wa Mjini Magharib Unguja na Chakechake Pemba.

Pia amezitaja sababu zinazopelekea maradhi ya mripuko kutokea mara kwa mara kama vile Upungufu wa kutotumia maji safi na salama,Uchafuzi wa mazingira tunayoishi,Utupaji ovyo wa taka na kinyesi cha binadamu ,Kutotumia vyoo kwa baadhi ya watu,Tabia za Uchafu wa miili na Mazingira machafu wakati wa kutayarisha chakula.

Nae Daktari dhamana Wilaya ya Mjini Ramadhan Mikidadi Suleiman amevitaja  vituo  vinavyo hudumia wagonjwa wa kipindu pindu ni Chumbuni Wilaya ya Magharib  na Gamba Mkoa wa Kaskazini A Unguja na Jumla ya idadi ya waliopata maradhi hayo ni 251 na 3 wamefiriki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Docter Ramadhan amesema kuwa kuna hatua mbali mbali wanazozichukua kama vile Ufatiliaji na elimu ya Afya kwa wagonjwa waliolazwa, Kufanya Uchunguzi wa maji katika makaazi, Elimu ya Afya kwa wananchi – Radio, mikutano ya hadhara, nyumba kwa nyumba, skuli nk .