Habari Mbaya: Mke wa Mzee Yusuf afariki Dunia

Aliyekuwa mfalme wa muziki wa Taarab Alhaj Mzee Yusuf amefiwa na mke wake Chiku Khamis Tumbo.

Chiku amefariki usiku huu katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua na kwa bahati mbaya yeye na mwanawe wamefariki.

Marehemu Chiku Khamis Tumbo

Mzee Yusuf amenukuliwa katika moja ya vyombo vya habari kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana leo saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na ikampoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.

Inna lillah wainna illayh rajiuwn…