Chidi Benz aibuka tena upya

Baada ya kujikomboa kutoka katika matumizi ya dawa za kulevya rapa Chidi Benz amejipanga upya ambapo wiki ijayo ataachia wimbo wake uitwao Muda akiwa amemshirikisha muimbaji Q Chief.

Ikiwa wiki ijayo Chidi Benz anarudi upya kwenye game mashabiki walikuwa wanamsubiria Chidi yule wazamani,” alisemaMeneja huyo. Mimi binafsi nje ya umeneja Chidi ni msanii ambaye namkubali sana toka kitambo.

Aliongeza, “Unajua ngoma nyingi za Chidi ambazo amekuwa akizitoa hivi karibuni sio level zake, lakini alivyonisikilizisha huu wimbo nimeona kuna kitu cha ziada kipo. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kuna jiwe linakuja,”

Meneja huyo amesema muda si mrefu wataanza kutangaza mfumo mzima wa uongozi wa rapa huyo.