Mashirikiano walimu na wazazi yahitajika

Wazazi na walezi kisiwani Pemba wametakiwa kutoa mashirikiano ya kutosha baina yao na walimu ili kumfanya mtoto kupata elimu itakayomuokoa katika maisha yake duniani na akhera.

Wito huo umetolewa na Mwalim msaidizi wa madarasatul siraji-munira ya Kilindi wilaya ya chakechake Ustadh Ramadhan Juma Ramadhan kwa kusema kuwa baadhi ya wazazi hawatoi  mashirikiano kwa walimu wa Madrasa pindi wanapowapeleka watoto wao chuoni.

Ustadh Ramadhan amesema ili kumfanya mtoto afanikiwe kielimu ni lazima kuwe na mashirikiano ya mzazi mwalimu na mtoto.

Nae Ustadh Khelef Haroub Abdallah wa madrasatul- Nurul-islamiya ya Shingi mjini chakechake ameungana na ustadh Ramadhani kwa kusema kua hakuna jambo kubwa linalorudisha nyuma maendeleo ya madarasa kama kutokuwepo mashirikiano baina wazazi na walimu kwa watoto wao.

Kwa upande wake Ustadh  Said Abdulrahman Muhammed kutoka Almadrasatul Khairia Islamia  amesema kuwa utandawazi uliyoingia nchini umechangia kiasi kikubwa kwa wazazi kutotoa mashirikiano kwa walimu.

Nae miongoni mwa mzazi wa wanafunzi Pandu Juma Zaid kutoka Msingini Chakechake amesema  kuna baadhi ya wazazi hawapotayari kutoa mashrikiano kwa walimu kwani kufanya hivyo kunarudisha nyuma sana maendeleo ya watoto.

Hata hivyo ametoa wito kwa wazazi kutilia mkazo suala la elimu, huku wakijua kua wanapompatia elimu bora mtoto ndio mafanikio katika dunia na akhera.