Sheikh Nassor aahidi kuishauri Ofisi ya mufti zanzibar kuwaendeleza wanafunzi wanaoshiriki mashindano ya Qur-an

Mhadhiri  wa chuo kikuu cha sumeit university Sheikh Nassor  Hamad Bakari, amesema ataishauri ofisi ya mufti zanzibar kuyashawishi mashirika makubwa ya kimataifa kuwaendeleza kielimu wanafunzi wanaohifadhi qur-ani.

Hayo  yamejiri kufuatia mashindano ya kuhifadhi qur-an yaliyofanyika katika msikiti mazuruy mombasa nje kidogo ya mji wa zanzibar.

Mashindano  ya qur-an imekua nijambo la kawaida na lilozoeleka hapa zanzibar kutokana na visiwa hivi kuwa na waisilamu wengi kwa asilimia karibu 99.9%  hali inayopelekea watu au mashirika ya kidini kufadhili mashindono ya qur-ani ndani ya zanzibar.

Mashindano  haya yamefadhiliwa na taasisi ya afrika muslim argency kutokana na fedha zilizo achwa na mbunge wa bunge lakuweit sheikh al-khurafy na kuamuru kutolewa wakfu kwa kutumika katika shughuli kama hizi.

Mkurugenzi  wa shirika la africa muslim argency iman mohammed kamal-din amesema utaratibu huu wa mashindano ya kuhifadhi qur-an utakua endelevu kulingana na mahitaji ya wanafunzi.

Mwanafunzi  salama omar wa al madrasatu imani islamia amesema wanawake wana nafasi kubwa ya kukihifadhi kitabu kitukufu cha qur-an pamoja na kukifanyia kazi.

Jumla  ya wanafunzi 25 wameshiriki katika mashindano hayo lakini mshindi wa mashindano hayo ni mwanafunzi yahya ali Abdallah aliyepata asilimia 100% katika kuhifadhi kwa njia ya tarteel, na amezawadiwa shilingi laki tano za kitanzania huku mshindi wa pili amezawadiwa shilingi laki nne na elfu khamsini wakati mshindi wa tatu akizawadiwa shilingi laki nne.

NA ABUBAKAR HARITH.