Sitti Mtemvu aahidi kueka ukweli kuhusu umri wake

Aliyekuwa Miss Tanzania Sitti Mtemvu amedai sakata la umri lililopelekea kuvuliwa taji la Miss Tanzania ni kitu ambacho kimebadili mfumo wa maisha yake kabisa huku akiwaahidi Watanzania siku moja kuweka wazi ukweli kuhusu umri wake.

“Mamshukuru Mungu maisha yanaendelea vizuri kwa sababu lile sakata lilikuwa kubwa sana lakini baada ya kumalizika niliamua kurudi shule na namshukuru Mungu nimemaliza salama na sasa anaendelea na shughuli zangu za kawaida,” alisema Sitti. “Ishu ya umri wangu siwezi kuizungumzia kwa sasa tuombe Mungu siku moja nitaanika ukweli na kila mtu anatajua ni nini kilitokea,”

Mrembo huyo kwa sasa anaendelea kufanya bishara ya kitabu chache cha Chozi la Sitti ambacho alikiandika baada ya sakata hilo.

Sitti alisema kitabu hicho kitaweza kuwasaidia vijana wengi hasa wakike katika nyanja mbalimbali za maisha.