Timbulo afurahia washirikiano anayopata

Mkali wa wimbo ‘Usisahau’, Timbulo amewashukuru mashabiki wa muziki bongo fleva kwa sapoti na upendo wanaomuonyesha kwa sasa.

Timbulo alisema kuwa anakiri kwamba nafasi aliyonayo kwenye muziki kwa sasa ni kubwa sana na upendo pia umeongezeka kuliko ilivyokuwa awali.

“Nashukuru kwa nafasi kubwa ambayo nimeipata kwenye game ya bongo fleva, nathubutu kusema sijawahi kupata toka mimeanza huu muziki, ‘this time’ naona ‘love’ imekuwa kubwa zaidi kuliko pale mwanzoni” Timbulo alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

Msanii huyo ameachia ngoma tatu mfuliluzo tangu mwaka uanze, alianza na ‘Usisahau’, ‘Mfuasi’ na sasa ameachia ‘Ndotoni’ huku akisisitiza kuwa bado ataendelea kuachia nyingine.