Simba wametoroka katika mbuga ya taifa Afrika Kusini

Simba wanne watoroka katika mbuga ya kitaifa nchini afrika kusini iitwayo Kruger  hali inayotia hofu kwa wakaazi wa karibu na maeneo hayo.

Simba hao walitoroka mbugani  mapeme  siku ya Jumapili na mara ya mwisho walionekana katika kijiji cha Matsulu.

Hadi sasa bado haijafahamika simba hao wametoroka kinamna gani hali yakuwa mbuga hiyo imezungushiwa uzio.

Aidha mnamo mwezi Mei Simba wengine watano waliripotiwa kutoroka mbugani hapo na wanne pekee walifanikiwa kupatikana ambapo mmoja wao hadi leo hajapatikana na hajulikani alipo.

Mbuga  ya  Kruger ni  mbuga kubwa zaidi barani Afrika yenye ukubwa wa kilomita 19.485 mraba.

Wahida Mbaya.