MC Pilipili apata ajali mbaya

Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias maarufu kwa jina la MC Pilipili amepata ajali katikati ya kijiji cha Nyasamba na Bubiki mkoani Shinyanga na kukimbizwa jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni dereva alipokuwa akijaribu kumkwepa mtoto aliyekuwa anaendesha baiskeli.