Bondia Anthony Joshua kutetea mataji yake oktoba 28.

BONDIA Anthony Joshua amethibitisha atatetea mataji ya ngumi za kulipwa uzito wa juu duniani ya vyama ya IBF, WBA na IBO kwa kupigana na Kubrat Pulev mjini Cardif, Oktoba 28.

Muingereza huyo aliunganisha mataji hayo baada ya kumpiga Wladimir Klitschko Uwanja wa Wembley Aprili 29, mwaka huu na amesema hawezi kuchelewa kumvaa Mbulgaria huyo kutetea taji lake.

Joshua amethibitisha kuwepo kwa pambano hilo baada ya Pulev kutangaza Jumatatu kwamba watapigana Uwanja wa Principality mjiniĀ Cardif, Oktoba.