De Boer afukuzwa Crystal Palace; Aweka rekodi

KOCHA Frank de Boer amefukuzwa katika klabu ya Crystal Palace .Kocha wa zamani wa timu ya taifa Uingereza Roy Hodgson anapewa nafasi kubwa kuchukua mikoba ya De Boer wakati wowote kuanzia hivi sasa.

De Boer anafukuzwa kutokana na matokeo mabaya, baada ya kushindwa kupata japo pointi au kufunga bao moja katika mechi nne za awali za Ligi Kuu ya England, ikiwemo ya Jumapili ambayo walifungwa na Burnley.

De Boer amekuwa kocha wa kwanza kutimuliwa nchini Uingereza msimu huu