“I Miss You” ngoma mpya ya Lady Jaydee

Malkia wa Bongo Flava Lady Jaydee,  baada ya kukaa kimya kwa takribani miezi mitano Jumanne hii ya tarehe 12, 9 ameachia wimbo wake mpya uitwao  ‘I Miss You’ ambayo imetayarishwa na Man Walter.

Akiongea na Bongo5, mmoja ya watu wa karibu wa msanii huyo amesema, video ya wimbo huo itatoka rasmi siku ya Ijumaa hii na imeongozwa na Justin Campos nchini Afrika Kusini.

Video ya mwisho ya Jide ilikuwa ni ‘Rosella’ aliyofanya na kundi la H_art The Band kutoka nchini Kenya ambapo pia wimbo huo unapatikana katika albamu yake mpya, Woman.