Nadal atwaa taji la Us Open 2017

Mchezaji nyota wa Tenis wa Hispania  Rafael Nadal ametwaa taji lake la tatu la Us Open baada ya kumfunga mcheza Tenis wa Afrika Kusini Kevin Anderson katika mchezo wa fainali kwa seti 6-3, 6-4. 6-4, kwa kutumia saa 2:30 katika dimba la Flushin Meadows.

Nadal ameifikia rekodi ya Roger federer ya kutwaa mataji matatu ya Us Open. Taji hilo linakuwa taji la 16 la mashindano makubwa ya Tenis aliyoshinda Nadal mwenye umri wa miaka 31.