SMZ yazindua laini ya simu maalum kwaajili ya Wazee.

Naibu Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Zanzibar Shadia Mohamed Suleiman amezindua laini ya simu ya mkononi  kwa ajli ya wazee wa Zanzibar  ili kuweza kuwasaidia  katika utoaji wa  taarifa  kwa haraka  pindi watakapopata matatizo kuhusiana na penshen jamii.

Akizungumza katika hafla ya  uzinduzi huo wa laini amesema kutokana na matatizo mengi yanayowakumba  wazee, serikali kwa makusudi  imeamua  kuzindua laini hiyo yenye namba 0774107070 kwa ajili ya kuwasaidia wazee kuweza kutoa taarifa popote alipo atakapopata matatizo ambayo wazee watatumia bure bila ya malipo.

Hata hivyo Shadia ametoa wito kwa  masheha pamoja na jamii inayowazunguka  kuwa na moyo wa kujitolea katika  kuwasaidia wazee ili kuwaondolea usumbufu.

Kwaupande wa wazee walio hudhuria katika uzinduzi huo wamesema wamefarajika kuona serikali imeweka mipango na mikakati imara kwa ajili ya kuwasaidia wazee  ikiwemo kuwasaidia huduma za mawasiliano ya bure kwa ajili ya kutoa taarifa zao.

Na:Amina Omar