Mahakama yatoa hukumu kwa Mataka wa ATCL

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka na mwenzake Elisaph Mathew, aliyekuwa Kaimu Afisa Mkuu kitengo cha fedha cha ATCL kulipa faini ya jumla ya sh. Milioni 70 ama kutumikia kifungo cha miaka sita jela. Pia mahakama imewaamuru kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo in USD 143,442.75.

Pia Mahakama imemuachia huru William Haji ambaye alikuwa ni Mkaguzi Mkuu wa hesabu za ndani za ATCL

Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Ndege Tanzania(ATCL),David Mataka akitoka katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu(Picha kutoka Maktaba)