Shamba la Yusuf Manji latiwa nguvuni na Serikali

Serikali imelifuta shamba la mfanyabiashara Yusuf Manji, lenye ukubwa wa eka 714, na waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.
Lukuvi amesema shamba lingine la kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa na kwasasa mashamba hayo yapo mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.
Hivyo Lukuvi amewaonya wananchi kuto kuvamia maeneo hayo na endapo mtu akivamia  na kujenga watamkamata na kumshitaki.“Muyaache maeneo hayo kama yalivyo mkijenga tutakuja kuvunja,” amesema.