Simu mpya inayotumia utambulisho wa uso badala ya kidole ili kufunguka yazinduliwa.

Kampuni ya Apple imezindua simu mpya aina ya iPhone X ambayo hutumia utambulisho wa uso wako badala ya kidole ili kufunguka na inauwezo wa kujichaji bila kutumia waya na haingii maji wala vumbi.

iPhone X ambayo inatumia utambulisho wa uso wako badala ya kidole kufunguka.

Apple imesema kuwa simu hiyo inayojulikana kama Iphone 10 pia inaweza kutumia utambulisho huo wa uso nyakati za usiku kufunguka na kwamba ni vigumu kuidanganya ikilinganishwa na mfumo wa kutumia kidole na ndio simu ghali zaidi kuzinduliwa na Apple.

Ikiwa na ukubwa wa kuhifadhi Gigabait 64 simu hiyo itagharimu £999 nchini Uingereza wakati itakapoanza kuuzwa rasmi mnamo mwezi Novemba tarehe 3 na Simu yenye ukubwa wa kuhifadhi Gigabait 256 itauzwa kwa £256 nchini Uingereza.

 

Mtaalam mmoja alisema kuwa uwezo wa Apple kuwashawishi wateja wake kugharamikia zaidi simu zake aina ya smartphone ni kitu cha heshima.