Wataalamu wamaliza maradhi ya kichocho Pemba

Timu ya watalamu wa afya kutoka nchi nane barani afrika wakishiriana na  madaktari bingwa kutoka   china kwa msaada wa shirika la afya ulimwenguni( WHO) wapo kisiwani Pemba kwaajili ya kupanga mikakati ya kumtokomeza kabisa konokono anaesababisha maradhi ya kichocho ilikumaliza ugonjwa huo visiwani zanzibar.

Wakizungumza katika mkutano wa siku nne unao fanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Pemba Misali Wesha nje kidogo ya mji wa Chake chake Mwakilishi wa Shirika la afya ulimwenguni WHO  Dr Alphoncia Nanai alisema shirika lake lina lengo la kutokomeza magonjwa 17 yasio pewa kipao mbele ikiwemo kichocho  mkakati ambao umelenga ifikapo 2020 uwe umekamiika

Alisema kwa mujibu wa utafiti ulio fanywa ugonjwa wa kicho cho unaweza ukamalizika kabisa pindi wakitokomeza mdudu konokono anae ishi kwenye maji ambae ndie anae zalisha wadudu wanao ambukiza ugonjwa wa kicho cho.

Alisema huo nimkutano muhimu wenye lengo la kujenga uwezo kwa nchi nane barani afrika ikiwemo tanzania ilikudhipiti waduduhao wanao pia kwenye ngozi na kuingia kwenye kibofu cha mkonjo kutoka kwa mdudu konokono.

Hivyo wameamua kutoa mafunzo ya namna ya kumtokomeza mdudu huyo konokono kwani hata wakitoa dawa kwa mgonjwa hupona ila  anarejea tena kwenye maji  naakakutana tena na mdudu huyo hupata tena magonjwa hivyo njia ya kudhibiti ugonjwa huo nikumuuwa kapisa konokono.

Kwa upndewake  Dr paulin mwenzi  wa shirika hilo kwa upande wa Kenya alizitaja nchi zilizo shiriki mkutano huo kuwa ni Kenya .Ithopia,  Gana, Uganda, Mozampiq, Ruwanda, Tanzania na wenyeji Zanzibar

Alisema sababu ya kuchaguliwa Zanzibar kuwa nisehemu ya majaribio kwa bara la afrika nikutokana utafiti ulio onyesha kuwa kichocho kimepungua sana hasa Pemba ambapo kama wakitokomeza vyanzo sababishi nidhahiri uwezekano wa kumaliza ugonjwa huo utapatikana.

Mkuu wa maabara ya Jamii kisiwani Pemba alisema licha ya kuwa kisiwa cha Pemba kinakabiliwa na  maeneo mengi yenye  maji  kama haya ya baridi ambapo mdudu huyu  konokono yupo na watu hasa watoto wana tumia sana  ila utafiti wao umeonyesha uwepo uwezekano wa mafanikio ya kumaliza ugonjwahuo wa kichocho kwasasa ulivyo pungua

Alisema wanaelewa kuwa Pemnba inamaeneo mengi ya mabwawa ya maji  yanayo tumiwa na watu na inavyanzo vingi ila wamekusudia Pemba kwavile mapitio ya awali yalionyesha kuwa asilimia 8 ya  watu wanaugonjwa ila baada ya kufanya matibabu sasa ni alsilimia mbili tu.

Mtaalamu kutoka nchini china Dr chenqeen chaciin amesema uzoefu walio pata kutoka china nikuwa dawa watakayo tumia kisiwani pemba nidawa salama kwa binaadamu baada ya siku tatu kuingizwa kwenye maji kuuwa vimelea vilivyomo kwenye konokono watu wanaweza kutumia maji hayo yakiwasalama bila ya madhara yoyote