Yatambue makubaliano ya Fumba town na PBZ.

Kampuni ya ujenzi wa nyumba za maendeleo katika kijiji cha fumba  (fumbo town development) imeingia mkataba  na Benki ya watu wa Zanzibar PBZ  ili kuwawezesha  wateja wa benki  hiyo kununua nyumba  kwa mkopo wenye  masharti nafuu.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya uwendelezaji wa mji mpya wa fumba Sebastian Dietzold amesema  wazanzibar wengi  bado hawajashajihika  na ununuzi wa nyumba za maendeleo  hivyo  makubaliano hayo  yaliyofikiwa  na  kampuni  hizo  yataweza kuwashajihisha wateja kununua au kukodi nyumba hizo zenye masharti nafuu.

Nae Mkurugenzi wa PBZ Juma Hafidhi Ameir amesema Benki ya PBZ ipo tayari kuwawezesha wananchi  wa Zanzibar  kuweza kumiliki nyumba ambazo ujenzi wake ni wanafuu  kwa kufuata utaratibu maalumu uliowekwa na  benk hiyo.

Mradi wa ujenzi wa nyumba za maendeleo fumba  unaoendelezwa na kampuni ya fumba town development unalengo la kuboresha maisha ya wananchi ili kuweza kuishi katika makaadhi bora na salama  pamoja na kuinua wananchi kiuchumi katika fursa za ajira.

Na:Amina Omar