Godbless Lema: Tundu Lissu hajashambuliwa na majambazi

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amedai kuwa tukio la Tundu  Lissu kushambiliwa kwa risasi lilipangwa na kikundi cha watu na sio majambazi kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Suala la Mh Tundu Lissu ni organized, ni mpango ambao umepangwa, Mh Lissu hajashambuliwa na majambazi, Mh Lissu alianza kusema anafuatiliwa siku nyingi na hata ukiangalia hilo jaribio la mauwaji yale lilivyotaka kufanyika unaona kabisa ni jambo lilipangwa vizuri kabisa, Mh Lissu ni mtu wa watu na wakati mwingine tunafanya vikao mpaka saa nane usiku kwahiyo kama shambulio la Mh Lissu lilikuwa lina lengo la kihalifu watu wangeweza kumsubiri akitoka Dar es salaam kuja Dodoma usiku, wangemsubiri jimboni kwake usiku lakini jambo hili limefanywa kutisha wazungumzaji wengine kama sisi, jambo hili ni lengo la kupeleka meseji kwamba tunaweza tufanya kitu chochote na msitufanye kitu chochote na unafahamu,” Lema aliiambia BBC.

Nae Mchungaji Peter Msigwa-mbunge wa Iringa mjini alisema bado afya ya Tundu Lissu haijaweza kukaa vizuri na bado yupo kwenye wodi ya watu wenye uangalizi maalumu.