Mabomu yatumika kutawanya wananchi Geita.

Polisi mkoani Geita wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi waliofunga barabara inayoelekea kwenye mgodi wa GGM kwa lengo la kulazimisha malipo ya kodi ya dola 12.

Tukio hilo limetokea mapema leo asubuhi ambapo pia madiwani wa eneo hilo na baadhi ya wananchi wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani humo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema bado hali ni tete, hivyo atatoa taarifa rasmi baada ya kuhakikisha hali ya kiusalama imetulia mgodini.