Kocha wa simba ajiuzulu

Kocha Jackson Mayanja ameamua kuachana na klabu ya Simba na kurejea kwao Uganda.

Mayanja ambaye bado yuko jijini Dar es Salaam, ameamua kuachana na Simba akidai ana matatizo yake binafsi.

“Ni matatizo ya kifamilia lakini suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa,” alisema.

Lakini habari kutoka Simba zimeeleza kuwa sasa wako katika hatua za mwisho kuvunja mkataba wake baada ya kukubaliana naye kutokana na uamuzi wake huo.