Rais Kenyatta amfungulia mashtaka Odinga

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemfungulia mashtaka ya kudharau Mahakama kiongozi wa Muungano wa Upinzani Nchini humo, Nasa, Raila Odinga.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Rais Kenyatta amefungua mashtaka hayo katika Mahakama ya Juu, ambapo Katibu Mkuu wa chama tawala cha Jubilee, Raphael Tuju, ameushutumu upinzani wa Nasa, kwa kutatiza mafunzo ya maafisa wa uchaguzi kwenye ngome kuu za Odinga magharibi mwa nchi hiyo.

Kesi hiyo ni mfululizo wa hali ya sintofahamu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa Urais Oktoba 26.