Awashambulia wazazi wake kwa imani ya kishirikina Mwanakwerekwe Unguja

Jeshi la polisi mkoa wa mjini Magharibi limemshikilia kijana mmoja Akramu Juma Nyange (28) kwa kufanya shambulio la watu watatu wa familia yake huko mwanakwerekwe.

Kwa mujibu wa taarifa Ya Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamanda msaidizi muandamizi wa Jeshi laPolisi Hassan Nassir ali amesema kuwa tukio hilo limetokea huko maeneo ya jitimai ya  zamani mwanakwerekwe amewashambulia mama mzazi,baba mzazi pamoja na mdogo wake na kuwasababishia maumivu makali kupitia kitu chenye ncha kali.
Ameongeza kusema kuwa chanzo cha tukio hilo kisingizio cha imani za kishirikina na huku mtuhumiwa huyo amekamatwa na yupo Kituo cha polisi na upelelezi wa shauri hilo na litakapo kamilika  atafikishwa mahakamani.
Hata hivyo Kamanda Nassir amewataka wananchi Kuacha kuamini imani za kishirikina ambazo ni potofu na baadala yake kufuata taratibu za kisheria
Tukio hilo limetokea leo asubuhii majira Ya saa 1 huko mwanakwere eneo la jitimai Ya zamani.
Na:Rauhiya Mussa Shaabani