Kiongozi ZFA mikononi mwa ZAECA kwa tuhuma za ubadhirifu

Mamlaka ya kuzuia rushwa na kuhujumu uchumi(ZAECA) wamemtuhumu Hassan Haji Silima  wa chama cha mpira wa mguu (ZFA) kwa  tuhuma za kuondoka na vitabu 3 vya risiti vyenye thamani Ya shilling laki tisa
Akizungumza na Zanzibar24 Msaidizi Mkuu wa Uchunguzi Ndugu Khamis Bakari Amani amesema kuwa mnamo tarehe 7 Ya mwezi huu wamepeleka jalada lake kwa Mkurugenzi wa mashtaka kwa ajili ya hatua za kisheria.
Ameongeza kusema kuwa mtuhumiwa huyo amechukua vitabu hivyo kila kitabu kimoja kina thamani shilingi laki tatu za kitanzania ambapo mtuhumiwa huyo amekiuka taratibu za kisheria  na matumizi mabaya ya mali na Mapato.
Aidha Khamis amewataka wanamichezo na watendaji wa michezo wawe waaminifu ili kuepuka lawama za hapa na pale na kufahamu kuwa mamlaka ya kuzuia rushwa na kuhujumu uchumi ipo macho na kuangalia kila nyanja kupitia taasisi mbali mbali kwa ajili ya kuhakikisha suala la rushwa linapungua na kuondoka kabisa ndani ya Zanzibar.