Snura kuifikisha Kampuni Mahakami

Marapa marafiki Ambwene Yesaya ‘AY’ na Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ wakiwa wamekaa mkao wa kula kusubiri mamilioni ya shilingi walizoshinda mahakamani kama fidia kwa kampuni moja kutumia wimbo wao bila idhini, Snura Mushi ambaye ni mkali wa Bongo Fleva, naye anatarajia kuiburuza mahakamani kampuni moja ya unga kwa kutumia wimbo wake wa Majanga kwenye matangazo yao bila makubaliano.

Snura alisema tayari mwanasheria wake amewapelekea ‘notice’ ya siku saba akiwataka kumlipa fidia ya shilingi bilioni 2.1 kwa kutumia wimbo wake bila idhini yake hivyo kama hawatajibu chochote kesi hiyo itapelekwa mahakamani.

“Kiukweli nimesumbuka kwa muda mrefu sana tangu mwaka 2015, nimewahi kuwatafuta wanasheria watatu ikashindikana, nikaenda COSOTA nako hakuna kilichoeleweka lakini kwa sasa nimepata mwanasheria mwingine ambaye naamini atafanikisha na nitapata haki yangu maana ushahidi na kila kitu kipo,” alisema Snura.