Mimba za umri mdogo zashika kasi Pemba

Imeelezwa kuwa mimba za umri mdogo zaongezeka kisiwani pemba hasa katika kipindi cha sikukuu ukilinganisha na miezi mengine.

Akithibitisha kutokea kwa matokeo tofauti katika mkoa wa Kusini Pemba kamanda wa polisi wa mkoa hua Shehan Mohammed Shehan amesema katika kipindi hicho matokeo kadhaa hujitokeza yakiwemo ya ubakaji, utoroshaji na mimba za umri mdogo.

Shehan amesema katika matokeo hayo tofauti kwa upande wa mimba za umri mdogo kwa mwaka 2017  katika maeneo ya Mazingwa Chakechake kijana Salum Yussuf (25) alimpa ujauzito mtoto mwenye umri (16) mkaazi wa Semewani  Chakechake  jina linahifadhiwa.

Magazeti ya Tanzania  Leo Jumamos November 11, 2017

Hata hivyo kamanda huyo amesema  mtuhumiwa wa kosa hilo alikiimbia na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta na kumpeleka kwenye vyomo vya sheria ili kujibu shitaka lake linalomkabili.

Kwa upande wa kesi za kutorosha Shehani amesema siku ya taarehe 06 mwezi  huu 2017 mtuhumiwa aliejulikana kwa jina moja la Yussuf wa Tironi mkoani alimtorosha msichana wa Tironi (16) alie chini ya wazazi wake ambapo ni kosa kisheria na mtuhumiwa huyo ameshakamatwa.

Nae mtuhumiwa aliejuilikana kwa jina moja la Is-haka alimtorosha msichana (17) alie chini ya ungalizi wa wazazi wake  wote wakaazi watironi mkoani na mpaka sasa mtuhumiwa huyo anatafutwa na jeshi la polisi ili kujibu tuhuma zinzomkabili.

Kamanda Shehan amesema mpaka sasa kwa wiki hii jumla ya matukio matatu yamefikishwa mahakamani yakiwemo ya utoroshaji , mimba za umri mdogo na ubakaji.

Ametowa wito kwa wazazi na walezi kwadhibiti watoto wao walio na umri mdogo kuanzia miaka kumi na sita hadi ishirini hususan kipindi cha sikukuu kufuatana na watu wazima ili kupunguza vitendo vya udhalilishaji vinavyokithiri siku hadi siku.

Nafda hindi.